Tangazo.com

Wednesday, October 9, 2013

JINSI YA KUTUNZA USO KWA WANAUME.

Ni jambo la kawaida kwa wanaume kutojali mambo yanayohusu urembo wakidhani ni kwa ajili ya wanawake tu, kitu ambacho si sahihi. Muonekano mzuri usoni kwa mwanaume kutokana na kujali vizuri ngozi na uso kwa ujumla.

Wataalamu wa masuala ya urembo wanasema wanaume wana wajibu wa kujijali katika sekta zote za urembo kama wanawake wanavyofanya bila kupata madhara ya aina yoyote.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ya kufanya katika kutunza uso ili uwe na muonekeno mzuri usoni:

Tumia visafisha uso (facial cleanser), japokuwa wanaume wengi hawapendi kufanya hivyo.

Takwimu zinaonyesha kuwa ni asilimia 15%tu ya wanaume hutumia njia hii kubiresha nyuso zao. Ndio maana wanaume wengi wanakuwa na mikunjo, madoa meusi, mbabuko katika ngozi zao.

Visafisha uso vinasaidia kutoa uchafu na mafuta yaliyozidi kwenye ngozi na kuacha ngozi yako ikiwa nzuri kabisa.

Kama uso wako una mafuta mengi basi tumia visafisha uso vyenye sabuni moja kwa moja au jelly lakini na kama uso ni mkavu tumia facial zenye mafuta.

Jenga utamaduni wa kusugua uso wako kwa kutumia scrubs aina ya Eden Apricot kwa sababu inachenga ndogondogo ambazo zitakufanya usiumie tofauti na zenye chenga nene.

Sugua uso wako angalau mara moja au mbili kwa wiki, hakika itasaidia kuondoa seli zilizokufa kwenye ngozi na kuifanya ngozi yako ya uso kuwa nadhifu na ya kuvutia.

Paka scrub hiyo ukizungusha uso mzima pasipo kuelekeza msuguo kushuka chini kwani unaweza sababisha nyama za usoni kushuka na hatimaye kukufanya uonekane mzee.

Safisha uso wako kwa maji baridi kisha paka losheni uliyozoea kuitumia hakikisha haiakisi mwanga wa jua kwa urahisi hasa kama ukijua unaenda kutembea juani ili kuzuia ngozi yako isiathiriwe na mionzi mikali ya jua.

Matumizi ya losheni pia yanategemea na aina ya ngozi yako mtu kama uso wako una mafuta mengi tumia zisizo na mafuta kama Nivea Milk itakayopunguza mafuta usoni ili uwezekano wa kutokwa na chunusi upungue.

Ukitaka kunyoa ndevu zilowanishe na maji ya uvuguvugu kwa dakika 1 au 2 kisha paka magic powder au krimu ya kuondoa ndevu iliyo na Vitamin E au Aloe vera .

Baada ya ndevu kulainika unaweza toa kwa kifaa maalum kisha paka After shave ili kuwezesha vinyweleo visivyokuwa vya lazima kutoka

Baada ya kumaliza hatua hiyo pakaa toner ili kuzuia vipele visiote na kusababisha muonekano mbaya usoni.

Kama huna uwezo wa kupaka toner au after shave unaweza tumia mafuta yoyote yatakayoweza kulainisha ngozi yako.

Tembelea saluni angalau mara moja kwa mwezi ili kusafisha uso wako kitaalam zaidi. Kufanya hivyo kutakusaidia kuondoa chunusi, mabaka meusi usiyoyapenda na vishimo vinavyotokana na chunusi zilizokomaa.

0 comments:

Post a Comment