Tangazo.com

Monday, January 6, 2014

Diamond Feat Davido - Number One Remix (Official Video)

                      

Sunday, January 5, 2014

Self Kuwa Feat. Fleah - Long Time (D.R.C) [Official Music Video]

                     

Subzilla - Nghelu (Official Video)

                      

Chege - Chapa Nyingine (Official Video)

                       

MUSIC | G VAN - NATAYA [OFFICIAL MUSIC VIDEO HD]

                  
                          

Saturday, December 21, 2013

MENINAH - SHAGHALA BAGHALA [Official Video HD]

                        

Saturday, December 14, 2013

MUSIC VIDEO | DAYNA NYANGE - MIMI NA WEWE.

                     
                       

Wednesday, December 11, 2013

ZITTO AWASHA MOTO CHADEMA


 
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema,Zitto Kabwe. 

Siku moja baada ya kuwasilisha maelezo yake ya utetezi baada ya kuvuliwa nyadhifa zake ndani ya Chadema, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe amekata rufaa Baraza Kuu kupinga hatua hiyo.
Zitto pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo walivuliwa nyadhifa zao na Kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Novemba 20 na 21 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana, Mwanasheria wa Zitto, Albert Msando alitaja sababu mbili za kukata rufaa kuwa ni kukiukwa kwa taratibu za kuchukua hatua za nidhamu na sababu zilizotolewa kutokuwa sahihi.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema mambo hayo yalishatolewa ufafanuzi na chama na kwamba kukata rufaa ni haki ya kikatiba kwa mwanachama yeyote.
“Kukata rufaa ni haki
ya kikatiba ya wanachama yeyote. Rufaa ikatwe tu, itashughulikiwa kwa mujibu wa katiba, kanuni, maadili na itifaki ya chama. Hata hivyo, ieleweke, rufani inahusu kuvuliwa nafasi za uongozi, kusudio hilo haliwaondolei wajibu wa kujieleza kwa maandishi mbele ya Kamati Kuu kwa nini wasifukuzwe uanachama,” alisema Mnyika.
Sababu za kukata rufaa
Akifafanua sababu za kukata rufaa, Msando alitaja kifungu cha 6.5.6 cha Kanuni ya Uendeshaji ya chama hicho, akisema utaratibu uliotakiwa kufuatwa kabla ya kumchukulia hatua za kinidhamu kiongozi kwa mujibu wa Katiba na Kanuni ni kupewa kwanza mashtaka kwa maandishi ili apate nafasi ya kujibu.
“Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashtaka yake kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashtaka kwa maandishi,” alisema na kuongeza:
“Kwa mujibu wa ibara ya 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.”
Alitaja vipengele vingine ni kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika na atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao ndani ya wiki mbili baada ya kusikilizwa.
Hata hivyo, kipengele ‘d’ kinasema: “Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu (b), (c) hapo juu kama itaona masilahi ya chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwanachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.
Alifafanua kuwa, siku ya kikao cha Kamati Kuu, Zitto hakupewa mashtaka yake bali aliyakuta ndani ya kikao baada ya kupewa taarifa kwa ujumbe wa simu (text message au sms). Zitto hakuwepo katika mkutano wa jana na waandishi wa habari.
“Kwa uzito wa makosa hayo yaliyosababisha kuvuliwa uongozi na kwa kuangalia athari zake kwake yeye binafsi na chama kwa jumla, Kamati Kuu ilitakiwa kujiridhisha kwamba kanuni za uendeshaji na katiba zinafuatwa,” alisema.
Mbali na Zitto, Msando alisema makosa hayo pia yalifanyika kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba. “Yeye hakuitwa kabisa kwenye kikao hicho na ni ukiukwaji wa Kanuni ya Uendeshaji 6.5.6(d),” alisema.
Aliongeza kuwa hata waraka wa mabadiliko ulioelezwa kuwa sababu ya Zitto kupewa adhabu hiyo haumtaji kabisa.
Akieleza nia ya Zitto kukata rufaa, Msando alinukuu katiba ya chama hicho ibara 6.3.6(d) na ibara 6.3.6(e) akisema:
“Kiongozi aliyechukuliwa hatua za kinidhamu na mamlaka yake ya nidhamu anayo haki ya kukata rufaa ngazi ya juu ya ile mamlaka yake ya nidhamu na uamuzi wa ngazi hiyo utakuwa wa mwisho”,” alisema na kuongeza:
“Huo ndio utaratibu ambao Zitto Kabwe ameamua kufuata kwa kuheshimu maamuzi ya Kamati Kuu lakini kukatia rufaa maamuzi hayo. Kuheshimu maamuzi siyo kuyakubali uhalali wake.”
Akana kuhujumu ziara ya Dk Slaa Kigoma
Katika hatua nyingine Msando alisema kuwa matukio ya vurugu yanayoiandama ziara ya Katibu Mkuu wa chama hicho mkoani Kigoma hayana uhusiano wowote na Zitto.
“Zitto Kabwe hahusiki kwa njia yoyote na hayo yanayoendelea na anayakemea na kuwashauri wanachama wote kuwa watulivu na kuendelea kuwaheshimu viongozi wa kitaifa,” alisema Msando.

TOP 5 YA VICHEKESHO VYA VUNJA MBAVU HIVI HAPA...SOMA UCHEKE HADI BASII NI NOMAAA.


  • Jamaa aliamua kumtoa demu wake out kwa ajili ya chakula cha usiku kufika hotelini wakakaa mezani muhudumu akaja,kaka nikuhudumie nini, tafadhali:NILETEE MENU LIST: dada na wewe,dada akajibu kwa pozi tena kwakujishaua,"NA MIMI NILETEE MENU LIST ILA CHUMVI WEKA KWA MBAAAAALI!
  • Hii Ni Kweli Ilitokea mitaa Fulani..na hata Ukicheki Sikuhizi wanaume huwa wanaendesha hovyo sana wanapoona wanawake wazuri/warembo mbele yao..
  • Ukikutana na Mwanamke mtata na ukamfanyia Upuuzi au Masihara Lazima Ujute maana Utapigwa Mangeu kama Huyu jamaa hapo chini... ni shidaaa



  • Ukitaka kujua mwanamke sio ndugu yako soma hii hapa upate undani. Jamaa karudi toka job mpole!
MKE: vipi leo mbona mapema na mpole?
MUME: ofisi yetu imeungua na watu wote wamekufa,
MKE: ilikuwaje wewe ukapona?
MUME: nilikuwa chooni, jirani na ofisi najisaidia.
MKE: Loh masikini familia zao itakuwaje?
MUME: watalipwa milioni 100 kila mfiwa.
MKE KWA HASIRA: ona sasa na wewe kunya kunya kwako umetukosesha mihela..ungeenda kunya akhera......
Ungekuwa Mwanaume Ungejibu Vip ?

  • DOGO KAULIZWA SWALI NA BABA YAKE Huku kaweka Sura ya Tabasamu...akajibu Ujinga....BABA alipogeuka na KUKAZA sura DOGO akarekebisha Kauli Ili yasimpate Mabaya...Nomaa Sana.. WAzazi Inabidi Kuwa Wakali Mara Nyingne...

Sunday, December 8, 2013

MWANAMUME AKIKOSA MTOTO HUPATA HUZUNI ZAIDI KULIKO MWANAMKE



 


Tofauti na mazoea na mtazamo wa wengi kwamba mwanamke ndiye anayeumia zaidi akikosa mtoto, wataalamu wamegundua kuwa anayeumia zaidi kwa kukosa mtoto ni mwanamume.
Utafiti huo umeonyesha kuwa wanaume wanahitaji mtoto sawa sawa na wanavyohitaji wanawake, lakini wao wanaumia zaidi wanapokosa bahati ya kupata mtoto.
Wataalamu hao wamebaini kuwa sababu kubwa zinazowafanya wanaume wajisikie vibaya zaidi wanapokosa watoto ni tamaduni za toka enzi kuwa wao wanaweza kila kitu na msukumo wa familia.
Tofauti na wanawake, ambao wanahitaji mtoto kwa ajili yao binafsi kwa asili ya kuumbwa kwao, hali ambayo kitaalamu inajulikana kama ‘biological urge’.
Taarifa za utafiti huo ulioongozwa na Robin Hadley, wa Chuo Kikuu cha  Keele, ukishirikisha wanaume 27 na wanawake 81, ambao hawajapata mtoto, uliwasilishwa mbele ya Wanasaikolojia wa Taasisi ya British Sociological Association,  ya Uingereza.
Waohitaji zaidi watoto
Kwa idadi hiyo waliosema wanahitaji watoto ni wanaume asilimia 59 na wanawake ni asilimia 63.
Nusu ya wanaume walisema kukosa mtoto kunawafanya waonekane tofauti kwenye jamii, huku wanawake wakisema wanahitaji watoto ili waje kuwasaidia baadaye.
Utafiti huo ulibaini kuwa asilimia 38 ya wanaume walihitaji mtoto kwa kuwa hawakuwa na mtoto kabisa, huku asilimia 27 tu ya wanawake ndiyo walikuwa hawana watoto kabisa.
Utafiti mwingine ulionyesha kuwa wanaume wanajisikia vibaya zaidi kukosa watoto kwa sababu asilimia ya wasio na watoto ni wanaume,tofauti na wanawake ambao wakati mwingine hubahatika kupata mmoja au wawili.
Tafiti hizo zilionyesha kuwa kati ya kila wanaume wanne  mmoja hana kabisa mtoto ikilinganishwa na asilimia 18 ya wanawake ambao hawana watoto.
Utafiti mwingine ulionyesha kuwa asilimia 56 ya wanaume hawana watoto kabisa, ikilinganishwa na asilimia 43 ya wanawake ambao hawana.
Akizungumzia utafiti wake Dk Hadley, anaeleza kwamba  amegundua kuwa kati ya wazazi wawili aliye kwenye hatari ya kukosa mtoto kabisa ni mwanaume, huku akiumia zaidi anapopatwa na hali hiyo kiasi cha kuwa na hasira, kujisikia vibaya mbele za watu, kujitenga na jamii, kuwa na wivu na mambo yanayofanana na hayo.
Wanawake kupenda watoto
Anabainisha kuwa hiyo ndiyo sababu inayowafanya wanawake wapende kupata watoto kuliko wanaume ili kuwaondoa kwenye matatizo hayo, ambayo mara nyingi husababisha familia nyingi kusambaratika bila kujali zilikuwa kwenye maelewano ya kiasi gani.
Alisema kwamba utafiti huo ulifanyika kwa njia ya kukusanya maoni kwenye mtandao, midahalo, kujaza dodoso za majibu na ulihusisha watu wenye umri wa kati ya miaka 20-66 huku wengi waliojibu maswali hayo walikuwa na umri usiopungua miaka 41.