Imebainika kwamba, wanaume wanaposaka wapenzi, huwa tayari kutii
masharti wanayopewa na upande wa pili. Utii huu ndiyo unaotajwa
kumvutia mwanawake kiasi cha kumfanya aamini kirahisi kuwa mwanaume wa
maisha yake ni huyo anayemtongoza wakati huo.
Hakuna shaka kwamba, katika mazungumzo ya awali ya mwanaume
anayemteka mwanamke kimahaba, kinywa chake huwa hakikauki maneno haya
manne zenye nguvu ya kumdatisha mwanamke, ambazo ni NAKUPENDA,
NAKUHITAJI, SAMAHANI na ASANTE.
Ni wazi kwamba kuna wanaume wengi ambao huanza na gia kubwa ya maneno
hao wamebainika kupoteza mvuto wa kimapenzi waliokuwa nao mwanzo kwa
wapenzi wao. Binafsi nathibitisha hili kwa kuwa nimeshafanya uchunguzi
kupitia wanaume wanaonijia kutaka majibu ya kwa nini wapenzi wao
wamewageuka na kutokuwapenda kama awali.
Kabla ya kuwashauri nimekuwa nawadodosa na hatimaye kutambua kuwa
waliacha kutumia maneno hayo mara tu walipoona amefanikiwa walichokuwa
wanakitafuta.
Kama nilivyosema neno la kwanza lenye nguvu ya kumteka kimapenzi
mwanamke ni NAKUPENDA. Neno hili ni tiba inayoponya hofu na kumfanya
mwanamke ajiamini.
Neno la pili, NAKUHITAJI. Kama inavyokuwa wakati wa kutongoza, mwanamke
anapenda kuambiwa neno hilo na kufanyiwa vitendo inavyoonesha kuhitajika
kwake katika maamuzi, matembezi, faraja na muongozo wa kimaisha.
Sambamba na hilo mwanamke anapenda sana kupewa ASANTE katika yale
anayofanya.
Jambo la mwisho kabisa ni SAMAHANI. Ndugu zangu kuna wanaume ambao
hawako tayari kuomba msamaha kabisa hata kama wamekosa kosa kubwa na la
wazi kiasi gani? Kifupi tabia hiyo haipendezi. Ni busara kwa mwanaume
kumuomba radhi mpenzi wake, ili naye ajione ni mwenye mamlaka na hivyo
kuzidisha upendo na uangalizi wa tabia mbaya za mwanaume.
Wednesday, December 4, 2013
MANENO MANNE MUHIMU YA KUTEKA PENZI LA MWANAMKE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment